Alikiba na nyayo kama za diamond ndani ya kigoma

0
Mapema Disemba 29,2019, Mwanmuziki Diamond na kundi lake la Wasafi pamoja na wasanii kadhaa walianza safari ya siku tatu kwenda mkoani Kigoma kwa njia ya treni na kufanikisha kukodi behewa kadhaa za treni kwa ajili ya safari hiyo kwenda kwenye tamasha la kurudi nyumbani kwa msanii Diamond.
Mwanamuziki mwingine anayefanya vizuri kwenye kiwanda cha Bongo Fleva Ali kiba anatarajia kuanza safari ya kwenda kufanya onyesho lake mkoani Kigoma na ameamua kutumia usafiri wa treni kama alivyofanya Diamond.
Alikiba ambaye pia ametangaza kuukodi behewa maalum kwa ajili ya kusafiri na wasani wenzie huku akiwataka mashabiki wanaopenda kusafiri naye mpaka Kigoma kumuunga mkono kwenye safari hiyo anayoitaka iwe ya kihistori.
Ali ameamua kulipachika jina la Ukarimu bahewa ambalo atalitumia kwenye safari hiyo kwenda kuwafurahisha wana kKigoma manamo Julai 31, 2020.

https://www.instagram.com/p/CC8ddUNBFMZ/?igshid=1r3uvesuet0u0

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here